Monday, 2 March 2015

TANGU NIINGIE KWENYE NDOA YANGU SISIKII HAMU YA TENDO LA NDOA KABISA

NIFANYEJE?
Anti kwanza kabisa naanza kwa kukupa pongezi katika kuelimisha jamii, mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 32 sasa lakini nina tatizo ambalo nimekaa nalo kwa muda mrefu sana bila kupata ufumbuzi, nimeolewa na nina watoto wawili tena mapacha na pia tunapendana sana na mume wangu kiasi kwamba watu wanatuonea wivu.

Anti ukweli wa mambo nimeona leo nikutobolee kwani ni siku nyingi nimetafuta msaada bila mafanikio lakini naona wewe mwanamke mwenzangu unaweza kunisaidia haswa na kunipa ushauri mzuri ambao utaniletea manufaa katika ndoa yangu.

Mimi na mume wangu kama ilivyo kawaida ya ndoa tunashiriki sana tendo la ndoa lakini anti ukweli ni kwamba simhisi kabisa mume wangu nafanya tendo la ndoa tu kama sheria hivyo kunilazimu mimi kutokusikia raha ya mapenzi.

Nashindwa kuelewa nimepatwa na kitu gani, nimejaribu kujichunguza na kugundua kwamba sina tatizo lolote nahisi kama nimelogwa anti mwenzio napata shida nipe ufafanuzi wa jambo hili niinusuru ndoa yangu kwani naona inakwenda mrama.

Jibu: Shosti kwanza kabisa nikupe pole lakini pia nikusifu kwa kuwa muwazi kwangu kwani si wote wanaopenda kuchojoa mambo yao ya ndani na wanapojaribu kufanya siri mambo ndipo yanapowaendea mrama na kujikuta wakiachiwa kwenye mataa au kutafutiwa mke mwenza nje ya ndoa hili si jambo zuri u kweli siku zote hata kama utakufanya upate aibu bado utakuwa umetatua shida zako kwa kiasi gulani. Unaweza ukawa na sababu mbalimbali lakini nitakupa nne tu ambazo ukizisoma na kuzielewa utafumbua tatizo lako.

Kutokufurahia tendo la ndoa kwa mwanamke ni ta tizo kubwa sana na sisi wewe tu wapo wengi lakini hupenda kufanya siri na huletwa na sababu mbalimbali.Pamoja na hayo yote vyanzo vingine ni magonjwa na matatizo ya kuzaliwa nayo haswa huchangia kwa kiasi kikubwa katika matatizo haya.

Kutokuweka akili yako katika tendo la ndoa hapa nina maana kwamba kichwa chako hufikiria mambo mengine mnapokuwa katika kushiriki tendo hili, akili yako haitulii katika kitu kimoja.

Zipo pia kero kutoka kwa waume zao, wanajikuta wanapoingia katika ndoa mambo huenda kinyume na tofauti wakati wa uchumba wao mwanaume huanza kubadilika kitabia kama alikuwa mpole basi huanza kuonyesha makucha yake hadharani Wakati wa uchumba au mapenzi kabla ya ndoa wengi hufurahia kwa kuwa kila mmoja wao hujaribu kuficha tabia yake lakini baada ya kuzoeana, tabia mbalimbali huanza kupungua mvuto wa kimapenzi na matatizo huanza kujitokea.

Mwanamke kutofurahia tendo la ndoa katika ndoa yake huchangiwa na matatizo ya kisaikolojia.

Hapana mwanaume anakuwa ameshaumia sana akili yake hivyo kufikiria zaidi nafsi yake kuliko kawaida hili nalo ni tatizo, kupoteza mapenzi kwa kiasi kikubwa nako pia huchangia tatizo hili
Wanawake wengine wakishagundua tabia za waume zao huchukizwa na tabia hizo uchafu hivyo inapofika mwanaume anataka tendo la ndoa mwanamke humwonea kinyaa anapofikiria tabia zake za nje hulazimika kufanya tendo la ndoa kwa kutimiza wajibu na sio starehe kama inavyotakiwa.

Naomba niliongelee jambo hili kwa kina zaidi kwa upande wa wanaume kwani baadhi yaao walio katika ndoa siyo waaminifu huwa na nyumba ndogo au wapenzi kiasi cha kushindwa kutimiza wajibu wao nyumbani hali hii huwaathiri wanawake kisaikolojia.

Mwanaume mkorofi kila anaporudi nyumbani yeye na pombe zake kichwani ni kuanza kumkong’oli mke wake tena mbele ya watoto wao jamani hii ni adabu kweli? Baadhi ya wanaume ni wagomvi na wakorofi kwa wake zao hivyo husababisha mwanamke aathirike kisaikolojia kwani kila akimuona mumewe huona kero na taabu inakuja.

Sababu za kiafya nazo pia huchangia sana jambo hili wakati mwingine unakuta mwanamke anaumwa na mwanaume anaporudi tu yeye ndio kazi bila kujali kwamba mkewe ana matatizo gani ndido maana nasema kwamba wakati tunapotenda tendo hili basi tuweke akili zetu katika hili na sio kufikiria maudhi.

TANGU NIINGIE KWENYE NDOA YANGU SISIKII HAMU YA TENDO LA NDOA KABISA Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin