Monday, 30 March 2015

SWAGA ZA WOLPER ZALETA KICHEFU CHEFU KWA BAADHI YA FANS WAKE!!

Kwa kawaida mitandao ya kijamii kama facebook, instagram, whatsapp , badoo, goole plus (g+) n.k imejizolea umaarufu mkubwa duniani na dhima kuu ya mitandao hii ni kupashana habari. Hii imekuwa ni fursa nzuri kwa watu maarufu kujiweka karibu zaidi na mashabiki wao hali imekuwa tofauti kabisa na inavyotegemewa katika nchi zetu zinazoendelea kwa mfano bongo.
Hali ya vijembe na maneno makali ya kashifa yanazagaa kwa kasi hasa mtandao kama wa instagram ambao hupendwa na vijana wengi kwa ajili ya kufanya mauzo si unajua tena mambo ya #SELFIE !!! na hivi visimu vya kupangusa (touch screen) ndo vimezua utata zaidi mtu selfie hadi chooni!!.


Basi mwanadada Wolper anayesumbua vyema kwenye tasnia ya bongo movie akatupia video hii hapo chini akiwa kaweka kipini kwenye pua yake duuuuh!! bonge la kosaa kwa wadau walio follow wenyewe kurasa yake pasipo shuruti wakamvagaa kwa maneno makali mara akaitwa "Iyo ereni puani tafkri ngombe,,"
mwingine akaibuka akisema "Nakukubali sana sister ila hizo swaga zako zinanichosha".VIDEO ILIYOLETA BALAA LOTE HII HAPA!!
Swali ambalo team michepuko inayojiuliza kama mtu anakuchefua ulitumwa um follow au utag mikorokocho yake tuache hizoo bwana!! (Hakununulii bundle kumbuka unajua hiyo mitusi unalipia wewe kwa washika dau wa vod* , au Tig* hahahha yeye mwendo mchibuyu hasara kwako).

SWAGA ZA WOLPER ZALETA KICHEFU CHEFU KWA BAADHI YA FANS WAKE!! Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin