Wednesday, 25 March 2015

MCHUNGAJI ANASWA LAIVU NA MKE WA MWANAJESHI,WAKUTWA GEST,ADAI NI MAOMBI TU


DUNIA inaelekea mwisho. Mchungaji mmoja wa Kanisa la Pentekoste, raia wa Kenya aitwaye Pasca Mugambi hivi karibuni alinaswa chumbani ‘live’ katika gesti moja iliyopo Manzese Tip Top akiwa na mke wa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambaye ni muunini wake, Risasi Mchanganyiko linakupa kisa kamili.

Mchungaji Pasca Mugambi akikosa la kufanya baada ya kufumaniwa.
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo kilicho karibu na mke wa mjeshi huyo kilisema kuwa mchungaji huyo alikuwa akifanya shughuli zake za maombezi mjini Dodoma na kwamba askari huyo alimuita ili ampe huduma za kiroho mama yake mzazi aliye mgonjwa, baada ya kuwa amefahamishwa kwake na rafiki yake mmoja.
“Mchungaji huyo alikuwa akiishi sehemu nyingine hapa Dar lakini akienda kila siku nyumbani kwa mjeshi huyo kumfanyia maombi mama yake. Sasa akiwa pale akavutiwa na mke wa jamaa akaanza kumtongoza, ikiwa ni pamoja na kumtumia picha zake mbalimbali za utupu, (tunazo),” kilisema chanzo hicho.
MKE ‘AMCHOMA’ MCHUNGAJI
Inadaiwa kuwa kitendo cha kutongozwa na mchunga kondoo huyo hakikumpendeza mwanamke huyo, ambaye aliamua kulifikisha suala hilo kwa mumewe ili wajue cha kufanya.
MJESHI AANDAA ADHABU NYEPESI
Chanzo chetu kinadai kuwa mwanaume huyo mwenye cheo jeshini, alimwambia mkewe kuwa asingependa kumuadhibu mchungaji huyo kwa kutumia cheo chake, badala yake akataka kushirikishwa kwa makamanda wa kitengo maalum cha Operesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers.
MJESHI AMWAGA UBUYU KWA OFM
“Huyu mchungaji nilimtoa Dodoma baada ya kupewa namba zake na rafiki yangu mmoja ili aje kumuombea mama yangu ambaye ni mgonjwa, lakini sasa namshangaa amepeleka maombi mengine kwa mke wangu, anamsumbua sana kuwa anampenda, nataka nimkomeshe ili iwe fundisho kwa wachungaji wengine wenye tabia kama yake,” mjeshi huyo aliwaambia makamanda wa OFM kwa njia ya simu.
MCHUNGAJI AINGIZWA KINGI
Baada ya kukubaliana na mumewe juu ya kumkomesha mkware huyo, mke alikubali ombi la mchungaji huyo (huku moyoni akiwa na lake jambo), mchungaji naye bila hiyana akajaa na kumuomba mwanamke huyo wakutane katika gesti hiyo tayari kwa kuivunja amri ya sita ya Mungu iliyo katika kitabu kitakatifu cha Biblia.
Mchungaji Pasca akiwa na muumini wake aliyenaswa nae.
MCHUNGAJI ATANGULIA GESTI
Akiwa na uchu, mchungaji huyo alitangulia ndani ya gesti hiyo (jina lake linahifadhiwa kwa sababu za kibiashara) na kupewa chumba namba 103 na kumtaarifu ‘bibie’ kuwa alikuwa tayari amefika.
MJESHI ABANA CHOBINGO
Wakati mawasiliano hayo yakifanywa, mjeshi huyo alikuwa na mkewe ‘chobingo’ wakiwasubiri makamanda wa OFM ambao walipoungana nao, mume huyo aliwatambulisha kwa mkewe na kuwapa mchongo mzima.
UTAMBULISHO WA FASTAFASTA
“Huyu ndiye mke wangu ambaye anasumbuliwa sana na huyo mchungaji, tulikuwa tunawasubiri mfike ili yeye aende chumbani kwa sababu tayari mchungaji ameshafika na anamsubiri,” alisema mjeshi huyo ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sababu maalum.
MWENYEKITI WA MTAA AITWA
Ili kwenda kisheria zaidi, OFM ilimtafuta Mwenyekiti wa Serikali wa mtaa huo aliyejitambulisha kwa jina moja la Mzee Mushi na kumpa mkanda kamili ambapo alikubali kutoa ushirikiano ikiwa ni pamoja na mmiliki wa gesti hiyo.
MCHUNGAJI AKUTWA NA BUKTA
Katika kundi lililowajumuisha wote hao, walifika chumbani hapo baada ya muda mfupi wa kusubiri na walipogonga, mlango ulifunguliwa na kuwakuta wawili hao wakiwa wamekaa kitandani na tayari wameshavua nguo zao za juu, mchungaji akiwa na bukta na fulana.“Mh! Hii ni aibu jamani yaani mchungaji kukutwa katika hali hii, waumini wataiga nini kwake?” alihoji mhudumu mmoja wa gesti hiyo.Akivaa baada ya fumanizi hilo.
ETI ALIKWENDA KUFANYA MAOMBI
Alipoulizwa na mwenyekiti sababu za kuwepo na mke wa mtu anayefahamiana naye, yeye akiwa mtumishi wa Mungu, mchungaji huyo alijibu kuwa aliombwa na dada huyo kumfanyia maombi.“Jamani naomba mnisamehe, shetani alinitangulia nilitaka kufanya maombi humu ndani,” alisema kwa kigugumizi mchungaji huyo.
MJESHI AMSAMEHE MCHUNGAJI
Katika hali ya ujasiri mkubwa, mjeshi huyo alimchukua mkewe na kumsamehe mchungaji huyo, lakini akamuonya kuachana na mchezo huo kwani anaweza kupoteza maisha yake

MCHUNGAJI ANASWA LAIVU NA MKE WA MWANAJESHI,WAKUTWA GEST,ADAI NI MAOMBI TU Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin