Sunday, 1 March 2015

JAMAA AKUTWA AMEKUFA HUKO MOROGORO MAITI YAKE YALIWA NA NYAU!Mwisho wa enzi! Jamaa mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Mbulu amekutwa kwenye jumba bovu akiwa amekufa kisha mwili wake kutoa harufu kali huku ukiliwa na paka.
Mwili wa Mbulu ukitolewa ndani ya jumba bovu.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, maiti ya jamaa huyo iligundulika wikiendi iliyopita katika jumba hilo maeneo ya Mtaa wa Simu B Kata ya Mji Mpya mkoani hapa ambapo wananchi wa maeneo hayo walisikia harufu kali kutoka kwenye jumba hilo, walipoingia ndipo wakakuta mwili wa jamaa huyo huku pua na sehemu za uso zikiwa zimetafunwa na paka.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mwenyekiti wa mtaa huo, Maneno Kifea ’Ticha’ alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.Licha ya harufu kali mwanahabari wetu alijitosa na kuingia kwenye jumba hilo ambapo alishuhudia mwili wa jamaa huyo ukiwa umeharibika.
...Mwili ukipakizwa kwenye gari.
Hata hivyo, serikali ya mtaa huo ilitoa taarifa polisi ambao walifika na kuuchukua kisha kwenda kuuhifadhi kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro huku uchunguzi ukiendelea juu ya kifo chake.  

JAMAA AKUTWA AMEKUFA HUKO MOROGORO MAITI YAKE YALIWA NA NYAU! Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin