Monday, 23 March 2015

BWANA WA WASTARA PAMOJA NA KUMTOSA WOLPER KIMAPENZI BADO BI DADA HUYO ANAAMPIGA MIZINGA MBAYA!!!



Mwigizaji Wastara Juma, akiwa na mume wake mtarajiwa Mark Edi.
Chanzo makini kilicho karibu na Mark ambaye ni mfanyabiashara mwenye maduka ya nguo jijini Dar, kimepenyeza habari kuwa, kabla ya kuanzisha uhusiano na Wastara, Mark alikuwa na uhusiano na Wolper lakini alimshindwa kutokana na tabia hiyo ya kupiga mizinga.
“Yaani Wolper ni balaa, anampiga sana mizingamizinga jamaa, mara anataka elfu 25, mara 30 yaani ni balaa tupu hadi ikafika steji Mark akaamua kumpiga chini na kutulia na Wastara,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kugaiwa ‘ubuyu’ huo sambamba na ushahidi wa SMS zilizoonesha Wolper akimuomba Mark fedha, mwanahabari wa Gpl  alimtafuta Mark ili kuweza kujua kama madai hayo yana ukweli ambapo alipopatikana alikiri na kudai amemchoka mwigizaji huyo.
“Daah! Umezipataje hizo habari? Ni kweli Wolper alikuwa mtu wangu lakini kwa sasa sina habari naye, ni mtu muongomuongo, mizinga kila wakati hadi nikaona bora niachane naye nitulie na Wastara,” alisema Mark ambaye kwa sasa wanapika na kupakua na Wastara.
via: Gpl.

BWANA WA WASTARA PAMOJA NA KUMTOSA WOLPER KIMAPENZI BADO BI DADA HUYO ANAAMPIGA MIZINGA MBAYA!!! Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin