Monday, 23 March 2015

ATHARI ZA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE (ATHARI ZA TIGO)


Sasa kama kawaida yangu mimi huwa sina tabia ya kutisha watu au kuwakataza bali najaribu kueleza ukweli kisha wewe kama mtu mzima utaamua nini cha kufanya kwani naamini kabisa kuwa sote ni watu wazima na tuna akili timamu na tunapoamua kufanya jambo sio kwamba tunafuata mkumbo au kulazimishwa bali ni our choice.

Kufanya ngono kusiko a.k.a Tigo “MWIKO” ktk jamii nyingi Ulimwenguni sio kwa vile tu inamaanika kuwa ni uchafu na inamadhara makubwa ya kimwili, kiakili na kiafya bali ni kinyume na mafundisho ya imani zetu za Dini.

Kinachofanyika chumbani ni uamuzi wenu ninyi wawili mnaopendana ikiwa tu mtakubaliana na kufanya hivo na pia ni siri yako wewe na mpenzi wako, kuna wapenzi wengi tunafanya mambo ya ajabu sana na watu tunaowapenda na tunafurahia na tunazidi kupendana na kutakana zaidi na zaidi kila siku….lakini mambo hayo ni “taboo” ktk jamii kama ilivyo kwa Tigo au Ukware/uzinzi.

Kuna baadhi ya watu (wake kwa waume) hujaribu na kisha wanajikuta wanafurahia na hivyo wanaendelea na kuna wengine hutaka kujua “unajisikiaje” lakini wanajikuta hawafurahii au mmoja wao hafurahii na hivyo wanaacha na kutorudia tena tendo hilo la mugongo-mugongo.

Inasemekana kuwa wanawake hatuna hisia za utamu au raha ndani ya tigo bali wanaume wanahisia Fulani na unono huko kunako “O” na baadhi husimamisha zaidi ikiwa watabonyezwa katikati ya korodani na sehemu ya kunyea au kuchuliwa/shikwa/kandwa/lambwa kwa vile kuna vijimishipa ambavyo ni “most sensitive”na hupelekea wapate utamu ule tunaoupata sisi wanawake tunapotandikwa kwenye “kipele G”. ……

Lakini kutokana na miiko wanaume wengi huwa hawaruhusu hii kwa vile wanahisi kuwa hakuna tofauti na kuwa shoga au wanadhani watazoea na kuwa “watoto wa watu” (Ushoga ni hali/hisia ya kuvutiwa/kutamani mtu wa jinsia yako sio kushikwa au kufurahia sehemu ya mwili wako).

Pamoja na kuwa watu kuheshimu miiko ya dini zao, kupinga na kulisema vibaya tendo hili wachunguzi wa mambo ya Tigo wanadai kuwa mwanamke mmoja kati ya wanne anashiriki ngono ya nyuma (sasa hii sijui ni kuridhisha wapenzi au ni wao wanafurahia)…….wazoefu watusaidie hapa.

Ukweli kuhusu Tigo.- Sio tendo asilia ktk swala zima la ngono na mapenzi hivyo kumbuka unapoamua kugawa tako kuwa na uhakika ndio kitu unataka kukifanya na sio kukifanya wa vile “mchumba” kaomba/anataka…..wewe ndio mwenye maamuzi makuu ya nini unataka kifanyike mwilini mwako. Kama unahisi unachokwenda kukifanya sio “natural” na hujisikii vema kushiriki ngono Tigo basi acha/kataa kufanya hivyo.

-tigo haina ute asilia wa kuusaidia uume kuingia bila “kwere” hivyo unahitaji vilainisho maalumu ili kurahisisha hilo.


- Hakikisha mnatumia Condom zenye “polyurethane” hizi inasemekana ni imara na zinahimili joto la huko kumavi kuliko zenye “spermicides” kwani husababisha muwasho utakaoweza kukusababishia maambukizo menine yayokanayo na wadudu asilia walioko sehemu hiyo ya kunyea.


-Mara mishipa ya tigo  ikitanuka kutokana na kufanywa huko mara kwa mara huwa haijirudi kama ilivyo kwenye uke kwa vile haikuumbwa kwa ajili ya shughuli hiyo.


-Hakikisha uume ukitoka tigo haugusi au kuingizwa tena ukeni ili kuepuka maambukizo kwani sote tunatambua kuwa huko mahala kuna vijidudu asilia ambavyo ukivikanganya tu unaibuka na gonjwa la ajabu(unakumbuka hadithi ya AIDS?).


-Wengi tunaamini kuwa kufanywa nyuma ni kwa mashoga tu lakini kuna wanawake wanafurahia kama ilivyo ngono ya mdomo na baadhi hujigeuza kama njia mbadala ya kuzuia mimba au kulinda bikira (zaidi ni ktk jamii ya waarabu).-Kuingiziwa ndude huko kumugongo kunauma (kunakupa maumivu)…..fikilia unapokunya kimba gumu tena baada ya kumeza mbegu za matunda Fulani yanaitwa “mabungo”…tunda lenyewe ni mbegu na mbegu hizo zinatabia ya kutereza bila taarifa…..sasa rafiki yangu sikilizia wakati wa kutoa kimba…utalia basi nasikia Tigo pia inauma sana lakini wasogo wake wanatumia mafuta au Jelly kutimiza haja zao.


-Ukizoea sana kupigwa nyuma na mishipa ya huko kutanuka, basi inasemekana kuwa utatatizwa wakati wa kujifungua/kuzaa, si hivyo tu bali unaweza ukawa na tatizo la kuvuja mkojo kwani hutoweza kukaza tena misuli yako ukeni ambayo hulegea baada ya kuzaa.

Swala muhimu sio kutisha watu bali kuwaelimisha na kuwaachia wao wachague mchele upi na pumba zipi. 
Ukiangalia yale yote yanayokatazwa au kuitwa miiko ndiyo yanayofanywa zaidi kuliko yale tunayoruhusiwa kuyazungumzia na kuyatenda.


*Mimi binafsi napinga kwa nguvu zangu zote swala la Ngono kusiko (tigo) ila na heshimu chaguo/uamuzi wako…..wewe ndio mweye mwili na unafanya vile utakavyo.

Ushuri wa bure-Jiheshimu na thamini mwili wako…..usitoe tako lako kama dawa ya kumfanya mume asitoke nje au akupende zaidi…..ni aibu mumeo akikuta nyuma jamaa waliwahi pia.

ATHARI ZA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE (ATHARI ZA TIGO) Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin