Wednesday, 18 March 2015

ACHOMWA MOTO NA WANANCHI BAADA YA KUMCHINJA MJOMBA WAKE HUKO MBEYA

mbeya
Tukio la mauaji limelotokea Mbeya, waliofariki ni mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitano ambaye ameuawa na mjomba wake, wananchi wenye hasira walimkamata mjomba huyo na kumuua pia.
Watu hao waliokuja eneo hilo walimkuta mjomba huyo akiwa amemuua mtoto huyo, wakaamua kumpiga mtoto mjomba huyo ana yeye mpaka akafariki, baadaye wakamchoma na moto.
Baba wa kijana huyo ambaye ni mjomba wa mtoto huyo amesema kijana huyo alikuwa na matatizo ya kifafa kwa muda mrefu.
Baadae wananchi hao walianza kuvamia nyumba hiyo iliyokuwa ikijengwa na kuanza kuivunja na kuiba vitu mbalimbali kwa kuhusisha ujenzi wa nyumba aliyouawa mtoto huyo na imani za kishirikina hadi Polisi walipofika na kupiga bomu la machozi kutawanya watu hao.
Fundi aliyekuwa eneo la tukio amesema mtoto huyo alifika eneo hilo wakawa wanazungumza nae, ghafla akatokea mjomba wake akiwa na fimbo akaanza kumuuliza maswali akakimbilia ndani kutafuta mlango wa kutokea, akamkimbiza na kumkamata wakasikia kelele na kuingia ndani wakamkuta kijana huyo akiwa na kisu mkononi na sururu akimchinja mtoto huyo, wakaanza kupiga kelele kuomba msaada wananchi walipofika wakaanza kumpiga na kisha kumchoma moto.

ACHOMWA MOTO NA WANANCHI BAADA YA KUMCHINJA MJOMBA WAKE HUKO MBEYA Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin