Friday, 27 February 2015

SHILOLE AWAFUNGUKIA MARAFIKI WANAOTAKA KUMGOMBANISHA NA NUH MZIWANDA


MSANII wa muziki na mwigizaji wa filamu za Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, ameamua kuweka wazi chanzo cha migogoro yake na mumewe mtarajiwa, Nuh Mziwanda kuwa ni marafiki.

Shilole alidai kuwa mara nyingi wamekuwa wakigombana, lakini chanzo kikiwa ni maneno ya uchonganishi kutoka kwa marafiki zao wa karibu ambao wana lengo la kuwatenganisha. Mwanadada huyo alidai kutokana na hali hiyo, hivi sasa ameamua kutowahusisha suala lolote linalohusu maisha yake ili kupunguza migogoro ya mara kwa mara baina yao.
Alisema wale walio karibu yao ndio wanaochangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa migogoro kwenye mahusiano yao, ukizingatia hivi sasa wapo kwenye harakati za kufunga ndoa baada ya wazazi wa pande zote kukubali uhusiano wao.

Tumegundua kuwa mashoga ndio wanaotugombanisha, kwani kila mara mchumba wangu anapewa taarifa zinazonihusu mimi huku hao hao wakiniletea habari zake, jambo hili limesabababisha nisihitaji tena marafiki wengi wao ni wanafiki,”alisema.

SHILOLE AWAFUNGUKIA MARAFIKI WANAOTAKA KUMGOMBANISHA NA NUH MZIWANDA Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin