Wednesday, 18 February 2015

DULLY AMLILIA BABAKE USIKU KUCHA


Na Chande Abdalah/Risasi Mchanganyiko
MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abdul Sykes maarufu kama Dully, Jumapili usiku alikesha akilia kiasi cha kushindwa kupokea simu kutoka kwa wadau mbalimbali waliompigia ili kumpa pole kwa msiba wa baba yake mzazi, Abby Sykes.
Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abdul Sykes maarufu kama Dully akiwa mwenye huzuni kubwa baada ya kufiwa na baba yake.
Mzee Sykes (63) alifariki akiwa hospitalini Muhimbili usiku wa Jumamosi na alitarajiwa kuzikwa Jumatatu jioni.
“Muda mwingi Dully alikuwa analia na kuna simu nyingi alishindwa kupokea, hasa za watu ambao alikuwa hajawasevu katika simu yake. Isingekuwa rahisi kwake kujibu kila aliyepiga kwa sababu wangeendelea kumliza,” alisema msanii mmoja aliyekuwa karibu na msanii huyo wakati gazeti hili likimtafuta ili kumpa pole. 

DULLY AMLILIA BABAKE USIKU KUCHA Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin