Friday, 20 February 2015

BREAKING NEWS: Taarifa ya msiba wa msanii wa BONGO FLEVA uliotokea leo Dodoma..

MEZ-B2


Moja ya taarifa ya kushtua na kuhuzunisha zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii, pamoja na watu kutumiana message ni kuhusu msiba wa aliyekuwa staa wa muziki wa Bongo Fleva, katika kipindi cha LEO TENA wametafutwa watu wa karibu ili kuthibitisha taarifa hiyo.
Dada wa marehemu ambaye jina lake ni Rachel amethibitisha kuwa msanii MEZ B amefariki akiwa nyumbani kwao Dodoma.
Noorah ni msanii ambaye walikuwa karibu na Mez B, amesema alikuwa akiwasiliana na Mez B ambaye alikuwa na homa tangu mwezi December mwaka jana na baadaye akasafiri kwenda Dodoma, mara ya mwisho wameongea kwenye simu ni siku tano zilizopita, leo simu yake imepokelewa na dada yake akimtaarfu kuwa Mez B amefariki muda mfupi uliopita.
Mez B aliwahi kuwa kundi moja Chamber Squad na akina Ray C, Noorah na marehemu Albert Mangwea pia.
Msiba uko nyumbani kwao eneo la Kisasa, Dodoma.

BREAKING NEWS: Taarifa ya msiba wa msanii wa BONGO FLEVA uliotokea leo Dodoma.. Rating: 4.5 Diposkan Oleh: Boss Ngasa

0 comments:

Post a Comment

LinkWithin